UFUGAJI BORA WA SAMAKI


Image result for ufugaji wa samaki

Ukuzaji viumbe kwenye maji ni miongoni mwa sekta zinazokuwa kwa kasi katika uzalishaji wa chakula duniani, pamoja na wingi wa pato lake bidhaa zinazozalishwa nchini zinaendelea, matarajio ya sekta hii ni kuendeleza michango yake katika usalama wa chakula na kupunguza umaskini. Hata hivyo, ni muhimu kwa juhudi za sasa kuwa mafanikio ya baadaye ya sekta katika nchi zinazoendelea na zilizoendelea, matatizo ya kijamii na kimazingira yanashughulikiwa ili kuhakikisha kwamba sekta hii inakuwa endelevu.

MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA UFUGAJI WA SAMAKI
yafuatayo ni baadhi ya mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya mjasiliamali hajaanza ufugaji wa samaki;
  1. 1.  KUWA NA MTAJI WA KUTOSHA
  2. 2.  KUTAYARISHA  ENEO BORA LA KUFUGIA
  3. 7.  KUTAYARISHA VIFARANGA BORA YA SAMAKI
  4. 3.  UPATIKANAJI WA CHAKULA CHA SAMAKI
  5. 4.  UWEPO WA MAJI SAFI NA SALAMA      
  6. 5.  ULINZI NA USALAMA WA SAMAKI
  7. 6.  SOKO LA UHAKIKA WA SAMAKI WAKO

JINSI YA KUANDAA BWAWA LA KUFUGIA SAMAKI
  •  Jambo la kwanza la msingi ni vipimo. Kimsingi  hakuna vipimo maalum vya ukubwa wa bwawa maana ukubwa wa bwawa unategemea eneo na malengo. Kwa mfanyabiashara bwawa kubwa litakuwa ni bora zaidi kwake ili aweze kuvuna samaki wengi zaidi ukilinganisha na mtu anayefuga kwa ajili ya chakula.
  •  Jambo la pili ni kuwa unapochimba bwawa unatakiwa kuchimba upande mmoja uwe na kina au umbali wa  mita 1.5 (mita moja na nusu) na upande mwingine mita 1 na sentimita 20 kwenda chini. Hii ni kwa sababu mianya ya jua ambayo inapeleka mwanga ardhini haiwezi kupenya kwenda chini zaidi ya mita 1.5 na hivyo ukizidisha zaidi ya hapo utakuwa umepoteza nguvu zako bure na ukipunguza utakuwa umeathiri ustawi wa samaki.
hatua ya kwanza ya uandaaji wa bwawa

  •  hatua ya pili ya uandaaji wa bwawa la samaki ni kulijengea,katika hatua hii ni muhimu kuwatafuta wataalamu walio na uzoefu wa kujenga na sio kila fundi ujenzi anaweza kujenga bwawa la samaki,kumekuwa na tabia ya baadhi ya wajasiliamali kwa kukwepa gharama huwachukua watu wasio na utaalamu,matokeo yake mabwawa mengi yanekuwa yakiwasumbua kwa kuvujisha maji,au kupasuka,kama hali ya uchumi hairuhusu ni heri ukaacha kulijengea bwawa lako ya kufugia samaki.

hatua ya pili ya uandaaji wa bwawa

  •  hii ni hatua ya mwisho katika uandaaji wa bwawa la kufugia samaki,katika hatua hii ni vyema kuhakikisha kwamba bwawa lako limejengwa vizuri na halivujishi maji,bwawa likiwa linapitisha maji ni hatari sana kwa usalama wa maisha ya samaki
hatua ya tatu ya uandaaji wa bwawa



 

No comments:

Post a Comment