KONA YA WAJASILIAMALI

Karibu sana katika blog hii,ambayo itakupa habari mbali mbali juu ya elimu ya ujasiliamali,kwanza kabisa watuwengi huwa wanajiuliza nini hasa maana ya ujasiliamali?na mtu ili aitwe mjasiliamali anatakiwa awe na sifa gani? hayo ni baadhi ya maswali ambayo watu wengi huwa tunajiuliza,majibu yake ni rahisi sana

NINI  MAANA  YA  UJASILIAMALI

Dhana ya Ujasiriamali ina maana pana , miongoni mwa hizo ni;  Mjasiriamali ni mtu ambaye ana hamasa kubwa ya kuleta mabadiliko chanya  katika hali yake ya kiuchumi ambaye ana tabia za kipekee ili kufanikisha azma yake hiyo kwa kujishuhulisha (yaani kujiajiri) ili awe na hali nzuri zaidi kiuchumi. 

Mjasiliamali ni mtu yoyote aliyeweza kuzitunia fursa mbalimbali zinazomzunguka katika mazingira yake ili kujipatia kipato


Kwa mitazamo mbalimbali ya wasomi wana muelezea  Mjasiriamali kama mtu ALIYEJITOA, ANAYEPANGA,MPUNIFU na ALIYE NA UTAYARI juu ya hatari zozote zinazoweza kujitokeza katika biashara/shughuli yake husika.  


SIFA ZA MJASIRIAMALI
 1. Mbunifu
hiki ni kitendo cha kubini au kutunga njia mbadala tofauti na zile zilizo zoeleka na watu wengi,kitendo hiki kitamfanya mjasiliamali kuweza kutoa huduma au kuwa na bidhaa tofauti zenye kuvutia katika soko hii itamfanya mjasiliamali kutanua soko na kuwa na wateja wengi.
 2.kuthubutu
 hiki ni kitendo cha ushujaa sana kwa mjasiriamali,hapa tunazungumzia uwezo na utayali wa  kufanya maamuzi ya kuingia katika biashara fulani au mradi fulani huku ukiwa umeondoa nidhamu ya woga. Watu wengi ni waoga wa kuchukua hatua au kuthubutu kuingia katika biashara,au mradi washwahili walisema:
 ''UWOGA WAKO NDIO UMASIKINI WAKO''
3. Jitihada
Mjasiriamali wakweli ni yule anachukua hatua bila kujali vikwazo wala matatizo, anatumia mbinu mbadala kuondokana na matatizo yanavyomkabili. Pia anatakiwa kuwajibika kutimiza lengo alilokusudia. Kimsingi mjasiriamali hachoki na wala hakati tamaa, muda wote akishindwa hili hufanya lile au kubadilisha mbinu ili afikie malengo.

4. Nidhamu
 Hii pia ni kanuni muhimu sana kwa mjasiriamali,mjasiriamali lazima awena na nidhamu katika biashara yake,awe na nidhamu katika matumiza yake ya pesa na ni lazima awe na nidhamu ya kufanya kakazi kwa bidii.nidhamu ni chanzo cha mafanikiao kwa kila mjasiliamali.

5.mshindani
mjasiliamali aliyekomaa haogopi ushindani wa kibiashara au kisoko,ni vyema kuzikabili changamoto mbalimbali zitokanazo na ushindani kutoka kwa wajasiliamali wengine kwani zitakujenga na kukufanya kutambua mbinu mbadala zitakazo kuimarisha na kuinua soko au biashara yako.

6. kupenda kujifunza
hii ni moja ya nguzo bora sana katika ujasiliamali,bila kujifunza hutoweza kusonga mbele katika shughuli unazo fanya,ni lazima kwa mjasiliamali kujifunza vitu vipya kupitia semina,makongamano,kusoma vitabu au majarida mbalimbali ili ajiongezee ujuzi utakao mfanya aweze kwenda sambamba na maendeleo haya ya sayansi na teknolojia.

7.kuwa na malengo 
malengo ni yale yote mjasiliamali anatarajia kuyapata kutokana na hicho alicho kikusudia kukifanya,ni vyema kwa mjasiliamali kuwa na malengo ya muda mrefu na yale ya muda mfupi,hii itamfanya mjasiliamali kuweza kufanya tathmini juu ya mwenendo wa biashara yake au shughuli anayoifanya.

8 Uaminifu
 Hii nayo ni tabia ambayo mjasiriamali anatakiwa kuwanayo,wateja wengi wanapenda mtu mwamifu na mkweli. Kama mjasiriamali ni lazima ufanye kazi yako katika mazingira ya uamifu na ukweli ili upate wateja wengi.Uongo katika biashara ni sumu ambayo itaua biashara yako.

NB;mjasiliamali ya kweli ni yule mwenye uwezo wa kubadili changamoto azipatazo katika shughuli zake za kila siku ili kuwa fursa, hii inamfanya awe mkomavu mwenye kuleta ushindani katika soko


 


No comments:

Post a Comment